• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Fedha za EAC kudhoofika dhidi ya dola ya marekani, Shilingi ya Kenya imebakia imara

    (GMT+08:00) 2018-06-18 20:08:58

    Sarafu za Afrika Mashariki, ikiwa ni pamoja na shilingi za Uganda na Tanzania na Franc ya Rwanda zimeendelea kudhoofika dhidi ya dola.

    Shilingi ya Uganda imeshuka chini na asilimia 3.6 dhidi ya dola tangu Januari wakati shilingi ya Tanzania imeshuka na asilimia 1.8. Franc ya Rwanda haijaathrika sana ilishuka kidogo tu kwa asilimia 0.9.

    Benki Kuu ya Uganda, imesema wiki iliyopita iliuza sh bilioni 101 ya dola mbali na ile iliyotarajiwa kuuzwa ambayo ni sh bilioni 180 baada ya kitengo kupoteza karibu Shs 50 ya thamani yake katika siku tatu tu.

    Kwa mujibu wa Benki ya Biashara ya Afrika, shilingi ya Kenya imebakia kuungwa mkono na ungiaji mzuri wa dola kutoka nje, lakini shilingi ya Uganda imekuwa chini ya shinikizo kutokana na mahitaji makubwa ya dola na sekta binafsi, nishati na benki za kibiashara .

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako