• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kikapu, Uganda: Kocha mpya wa timu ya taifa aandaa mkakati wa ushindi

  (GMT+08:00) 2018-06-19 09:32:56

  Kocha mkuu mpya wa timu ya taifa yaUganda ya mchezo wa mpira wa kikapu, George Galanopoulos amedai kubaini mapungufu yaliyopo kwenye timu hiyo, na kwamba tayari ameanza mkakati wa kuyatatua kabla ya kuanza kwa raundi ya pili ya mechi za mchujo za kufuzu kombe la dunia mwaka 2019.

  Ukosefu wa uzoefu kwa baadhi ya wachezaji, na kukosekana kwa wafungaji madhubuti katika timu hiyo, ni miongoni mwa sababu zilizotolewa na kocha George ambaye sasa anaiandaa timu hiyo kuelekea mechi za mchujo baadaye mwezi huu.

  Timu ya Taifa ya Uganda imecheza mechi mbili za majaribio, ambapo jumapili ilicheza na Iraq ikaibuka na ushindi wa alama 90-72, na jana jumatatu ilipofungwa na Saudi Arabia kwa alama 90-66.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako