• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania yachukua tahadhari kuhusu homa ya Rift Valley

    (GMT+08:00) 2018-06-19 09:53:25

    Tanzania imetoa tahadhari baada ya mlipuko wa homa ya Rift Valley RVF kuibuka nchini Kenya na Rwanda.

    Katibu mkuu wa wizara ya mifugo na uvuvi, Bibi Mary Mashingo amesema serikali imezielekeza halmashauri za wilaya, manispaa na miji ili kuhakikisha umma unaelimishwa kuhusu homa hiyo, ambayo imesababisha vifo vya watu 6 nchini Kenya.

    Amesema mpaka sasa hakuna maambukizi ya homa hiyo kuripotiwa nchini Tanzania. Pia ameelekeza halmashauri hizo kuhakikisha kwamba wanyama wote wanapelekwa kwenye machinjio maalum ambapo wapo wataalamu wa mifugo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako