• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wawili wauawa katika mapigano kati ya wakimbizi kutoka Sudan Kusini nchini Uganda

    (GMT+08:00) 2018-06-19 17:20:46

    Wakimbizi wawili kutoka Sudan Kusini wameuawa katika mapigano ya kikabila yaliyotokea wilayani Arua, mkoa wa West Nile, kaskazini magharibi mwa Uganda.

    Msemaji wa polisi mkoani humo Josephine Angucia amesema, watu wa wawili kutoka kabila la Dinka waliuawa katika mapigano na watu wa kabila la Nuer. Mapigano hayo yalitokea wakati wakiangalia mechi ya Kombe la Dunia katika kambi ya wakimbizi ya Rhion iliyoko ukanda wa Tika.

    Angucia amesema, ofisi ya Waziri Mkuu wa Uganda imeanza mchakato wa kutenganisha makundi hayo mawili kwa kuwahamishia kwenye kambi nyingine tofauti. Amesema kwa sasa hali ni tulivu na polisi wamepelekwa kwenye kambi hiyo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako