• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China afanya mazungumzo na Rais wa Bolivia

    (GMT+08:00) 2018-06-19 19:51:29

    Rais Xi Jinping wa China amefanya mazungumzo na Rais Evo Morales wa Bolivia kwenye Jumba la Mikutano la Umma hapa Beijing, ambapo marais hao wameamua kuanzisha ushirikiano wa kimwenzi wa kimkakati kati ya China na Bolivia na kukuza uhusiano wa nchi hizo mbili kuendeleza zaidi katika hatua mpya ya kihistoria.

    Rais Xi amesisitiza kuwa, nchi hizo zinatakiwa kuwa wenzi wa maendeleo, kuimarisha ushirikiano wa kimkakati wa maendeleo chini ya mfumo wa " Ukanda Mmoja na Njia Moja" na kujenga mfano mpya wa ushirikiano katika uwekezaji, biashara na huduma kwa pamoja. Amesema China ina msimamo wazi wa kuingiza bidhaa zaidi za kilimo na ufugaji wa Bolivia.

    Kwa upande wake, rais Morales amesema, China daima inaunga mkono na kusaidia maendeleo ya uchumi, jamii ya Bolivia bila masharti ya kisiasa. Amesema Bolivia ina imani na pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja la China, na ina nia ya kujenga pendekezo hilo pamoja na China na kuimarisha ushirikiano katika kila sekta.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako