• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China afanya mazungumzo na kiongozi wa Korea Kaskazini

    (GMT+08:00) 2018-06-19 21:05:27

    Rais Xi Jinping wa China leo hapa Beijing amefanya mazungumzo na kiongozi wa Korea Kaskaini Bw. Kim Jong Un ambaye yuko ziarani nchini China.

    Viongozi hao wamebadilishana maoni kuhusu maendeleo ya uhusiano kati ya nchi hizo mbili na hali ya peninsula ya Korea, na kufikia maoni ya pamoja kuhusu kuimarisha uhusiano kati ya nchi hizo, kuhimiza amani na utulivu wa peninsula ya Korea, na kutoa mchango kwa ajili ya amani, utulivu na ustawi wa kikanda na wa kimataifa.

    Bw. Kim Jong Un amesema mkutano wa viongozi wa Korea Kaskazini na Marekani uliofanyika hivi karibuni ulipata mafanikio yanayoambatana na maslahi ya pande mbalimbali na matarajio ya jumuiya ya kimataifa. Kama Marekani na Korea Kaskazini zikitekeleza kihalisi maoni ya pamoja yaliyofikiwa na viongozi wao, itafungua ukurasa mpya wa suala la kutokuwepo kwa silaha za nyukilia kwenye peninsula ya Korea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako