• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Katibu Mkuu wa UM atoa mwito wa kuwepo kwa umoja, kujali na kuchukua hatua

    (GMT+08:00) 2018-06-20 08:46:10

    Leo tarehe 20 Juni ni siku ya wakimbizi duniani. Wakati dunia ikiadhimisha siku hii katibu mkuu wa Umoja Bw. Antonio Guterres ameitaka dunia nzima kufikiri ni nini kinachoweza kufanyika ili kuwasaidia wakimbizi, kwa kuanza na umoja na mshikamano.

    Amesema leo kuna wakimbizi na wakimbizi wa ndani milioni 68 duniani, idadi ambayo ni sawa na nchi ya 20 kwa ukubwa duniani. Mwaka jana wastani wa mtu mmoja alipoteza makazi katika dakika mbili, hasa kwenye nchi maskini.

    Bw. Guterres amesema anasikitishwa sana kuona wakimbizi hawapati ulinzi wanaohitaji na wanaostahili.

    Pia amesema mwaka huu makubaliano ya dunia nzima kuhusu wakimbizi yatawasilishwa kwenye baraza la umoja wa mataifa, yakitoa njia ya kutambua mchango unaotolewa na wakimbizi katika jamii zinazowapokea.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako