• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • UNICEF yasema watoto hawatakiwi kupokwa kutoka kwa wazazi wahamiaji

    (GMT+08:00) 2018-06-20 08:46:29

    Shirika la kuhudumia watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limesema watoto hawatakiwi kupokwa kutoka kwa wazazi wahamiaji, kama inavyofanywa kwenye hatua yenye utata inayochukuliwa na serikali ya Marekani kwenye mpaka wake na Mexico.

    Mkurugenzi wa UNICEF Bibi Henrietha Fore amesema habari za watoto, baadhi yao wakiwa vichanga, kutenganishwa na wazazi wao wanaotafuta usalama nchini Marekani zinasikitisha. Amesema watoto, bila kujali wanatoka wapi na kama ni wahamiaji au la, bado ni watoto.

    Kauli ya Bibi Fore inafuatia hatua zilizochukuliwa na serikali ya Marekani kwa muda wa wiki sita sasa, na kushuhudia watoto zaidi ya 2,000 kuchukuliwa kutoka kwa wazazi wao walioingia nchini Marekani kutoka Mexico kinyume cha sheria. Watoto hao wamewekwa kizuizini kusini magharibi mwa Marekani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako