• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jeshi la Yemen latwaa udhibiti uwanja wa ndege wa Hodeidah

    (GMT+08:00) 2018-06-20 09:10:17

    Wizara ya ulinzi ya Yemen imesema jeshi la serikali ya Yemen limekamilisha operesheni ya kuwaondoa wapiganaji wa kundi la Houthi katika uwanja wa ndege wa Hodeidah na kutwaa udhibiti kamili wa uwanja huo.

    Wizara hiyo imetoa taarifa ikisema kamanda wa jeshi la serikali ya Yemen katika operesheni ya mji wa Hodeidah Bw. Abu Mouhrrami ametangaza kuwa jeshi lake lilipambana vikali na wapiganaji wa kundi la Houthi waliosalia na kujificha kwenye uwanja wa ndege wa Hodeidah, na kufanikiwa kuudhibiti uwanja huo kikamilifu.

    Habari pia zinasema majeshi ya muungano yalifanya shambulizi la anga kwenye uwanja huo na kuwaua makumi ya wapiganaji, na kuwalazimisha wengine kukimbia.

    Wakati huo huo, mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa anayeshughulikia suala la Yemen Bw. Martin Griffiths ameondoka Yemen bila kufanikisha usuluhisho na kundi la Houthi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako