• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kombe la Dunia: Senegal yapata ushindi, yatoa matumaini Afrika

    (GMT+08:00) 2018-06-20 10:15:59

    Senegal jana imeanza vyema kampeni zake kwenye michuano ya kombe la dunia baada ya kuifunga Poland kwa magoli 2-1 mjini Moscow.

    Senegal inakuwa timu ya kwanza kwa Afrika kupata ushindi katika michuano hiyo baada ya timu zingine nne kufungwa kwenye mechi zake na sasa ili kufuzu hatua ya 16 bora inahitaji ushindi walau mara moja katika mechi zake mbili za hatua ya makundi dhidi ya Japan Juni 24 au Colombia Juni 28.

    Lakini kwingineko katika mechi zilizopigwa jana, Misri imefungwa na wenyeji Urusi, na kwa kuwa ni kipigo cha pili mfululizo ni wazi kuwa watayaaga mashindano hayo kwa kuwa Uruguay ambayo inacheza leo dhidi ya Saudi Arabia ina nafasi kubwa ya kusonga mbele.

    Kwingineko wenyeji Urusi wamekuwa timu ya kwanza kufuzu hatua ya 16 bora ya mashindano hayo baada ya kupata ushindi wa pili mfululizo kwa kuifunga magoli 3-1 Misri jana.

    Katikamechi zitakazopigwa leo, Morocco inacheza na Ureno, Saudi Arabia na Uruguay, na Iran itakuwa kibaruani dhidi ya Hispania.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako