• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tamasha la utalii la Njia ya Hariri lafunguliwa mkoani Gansu

    (GMT+08:00) 2018-06-20 17:28:46

    Tamasha la utalii linaloonyesha ushirikiano kati ya nchi zilizo kwenye Njia ya Hariri limeanza jana mkoani Gansu, kaskazini magharibi mwa China.

    Wageni 1,500 kutoka nchi na sehemu 52 walihudhuria hafla ya ufunguzi wa Tamasha la 8 la Utalii la Kimataifa la Njia ya Hariri, ambalo litamalizika Julai 20.

    Kwa muda wa mwezi mmoja ujao, miji ya mkoa wa Gansu itafanya matamasha 55 ya kiutamaduni, ambayo yanatarajiwa kuvutia watalii milioni 34 na kuingiza kiasi cha dola za kimarekani bilioni 3.64.

    Tamasha hilo linaloandaliwa kwa pamoja na Wizara ya Utamaduni na Utalii na serikali ya mkoa wa Gansu lilianza mwaka 2011, na limekuwa jukwaa muhimu la kuhudumia nchi za Njia ya Hariri na kwa miji ya China kubadilishana maoni kuhusu utalii.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako