• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yasikitishwa na Marekani kwa kujitoa kwenye Baraza la haki za binadamu la Umoja wa Mataifa

    (GMT+08:00) 2018-06-20 17:29:47

    Balozi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Bibi Nikki Haley jana ametangaza kuwa Marekani itajitoa kwenye Baraza la Haki za Binadamu la Umoja wa Mataifa.

    Akizungumzia hatua hiyo, msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Geng Shuang leo hapa Beijing amesema, China inasikitishwa na uamuzi huo wa Marekani, na kusisitiza kuwa siku zote China inafanya juhudi na kulinda siasa ya pande nyingi na kuliunga mkono Baraza la haki za binadamu kuhimiza na kulinda haki za binadamu duniani.

    Wakati huo huo, Bw. Geng amesema China itashirikiana na pande mbalimbali, kutoa mchango kwa maendeleo ya majukumu ya haki za binadamu za kimataifa kwa kupitia mazungumzo ya kiujenzi na ushirikiano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako