• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Russia yatangaza kuongeza ushuru kwa bidhaa za nje za Marekani

    (GMT+08:00) 2018-06-20 18:31:12

    Waziri wa Maendeleo ya Uchumi wa Russia Bw. Maksim Oreshkin amesema, kutokana na hasara zitakazoletwa na hatua za kujilinda kibiashara za Marekani kwa Russia, nchi hiyo itaongeza ushuru wa forodha kwa baadhi ya bidhaa zinazoagizwa kutoka Marekani, na orodha ya bidhaa halisi itatangazwa katika siku chache zijazo.

    Waziri Oreshkin amesisitiza kwamba, Russia itaongeza ushuru kwa bidhaa za nje za Marekani zilizo na bidhaa mbadala kwenye soko la Russia, hivyo haitaathiri maendeleo ya uchumi wa Russia.

    Serikali ya Russia imeandika barua kwa Shirika la Biashara Duniani (WTO) mwishoni mwa Mei, ikisema Marekani imeongeza ushuru kwa bidhaa za chuma na aluminium za Russia na kusababisha hasara ya dola za kimarekani milioni 537.6 kila mwaka kwa Russia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako