• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Uganda yajipatia fedha zaidi za mauzo ya kilimo nje

    (GMT+08:00) 2018-06-21 18:53:41

    Uganda imeendelea kujipatia fedha zaidi kutoka kwa mauzo ya bidhaa za kilimo mwaka huu.

    Baada ya kikao cha kujadili bei ya nafaka zinazonunuliwa na wafanyabishara wa nchi nyingine za Afrika Mashriki,takwimu zinayonyesha Uganda mwaka huu itaongeza zaidi ya asilimia 12 za mauzo ya chakula.

    Chris Kaijuka, Mwenyekiti wa baraza la nafaka nchini Uganda amesema wameuza mahindi kwa bei nzuri msimu huu.

    Mwaka huu Uganda hadi sasa imeuza karibu tani 38,000 za mahindi za thamani ya dola milioni 15 kwa nchi jirani kwa nusu bei ya ile ya kimataifa.

    Rwanda kupitia kwa mipaka ya Gatuna na Cyanika imenunua tani 5,405 ikifuatiwa na DRC ambayo imenunua tani 1,105 kupitia mipaka Rusizi, Mpondwe na Rubavu huku mayo Tanzania ikiagiza tani 480.

    Wafanyabiashara wananunua mahindi kutoka maeneo ya Tororo, Gulu, Masindi na Lira kwa bei ya dola 180 kwa tani moja lakini nchini Kenya tani moja imefikia dola 430.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako