• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tamasha la tatu la vijana wa China na Afrika lafanyika Beijing

    (GMT+08:00) 2018-06-21 19:21:40

    Tamasha la tatu la vijana wa China na Afrika limefunguliwa leo hapa Beijing ili kutathmini maoni ya pamoja yaliyofikiwa kwenye mkutano wa Johannesburg wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika, na kuandaa mkutano wa kilele wa baraza hilo utakaofanyika mwezi Septemba hapa Beijing.

    Watu zaidi ya 400 wakiwemo wajumbe wa vijana wa China na Afrika, mabalozi wa nchi za Afrika nchini China, wajumbe wa wanafunzi wa Afrika wanaosoma nchini China, na wajumbe wa mashirika ya habari ya China na Afrika wameshiriki kwenye ufunguzi wa tamasha hilo la siku 8

    litakalofanyika katika miji ya Beijing na Chengdu.

    Lengo lake ni kuwawezesha vijana wa Afrika kuona mafanikio ya China tangu ilipoanza kufanya mageuzi na kufungua mlango wa nje miaka 40 iliyopita, na matokeo ya ushirikiano wa kiuchumi na kibiashara kati ya pande hizo mbili, kuimarisha mawasiliano kati ya vijana wa China na Afrika, na kuzidisha urafiki kati yao

    Bi. N eema Protas Matheleka kutoka Tanzania amesema, kupitia tamasha hilo, vijana wa Afrika wanaweza kuiga uzoefu wa maendeleo ya China, na kutoa mchango kwa maendeleo ya nchi zao.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako