• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tamasha la pili la kimataifa la filamu la China na Afrika kufanyika Cape Town mwezi Oktoba

    (GMT+08:00) 2018-06-22 19:01:08

     

    Tamasha la pili la kimataifa la filamu la China na Afrika linaloandaliwa kwa pamoja na Kituo Kikuu cha Radio na Televisheni cha China na chuo kikuu cha filamu cha Beijing linatarajiwa kufanyika mwezi Oktoba mjini Cape Town, Afrika Kusini.

    Akizungumza kwenye mkutano na waandishi wa habari kuhusu uzinduzi wa tamasha hilo uliofanyika mjini Shanghai, mhariri mkuu wa Redio China Kimataifa Bw. Ren Qian amesema, hii ni mara ya kwanza kwa kituo hicho kuandaa tamasha la kimtaifa la filamu katika nchi ya nje tangu ilipoanzishwa, na pia imeonesha urafiki kati ya China na nchi za Afrika.

    Mkurugenzi wa masoko wa tamasha hilo Bw. Jehad Kasu amesema, kwa kupitia tamasha la filamu la China na Afrika, watu wa China na Afrika wanaweza kuelewana zaidi kuhusu utamaduni wao. Licha ya Afrika Kusini, maonesho ya filamu yatafanyika katika nchi nyingine barani Afrika.

    Kituo Kikuu cha Radio na Televisheni cha China ni chombo kikubwa zaidi cha redio na televisheni, pia ni chombo cha habari cha kimataifa kinachotumia lugha nyingi zaidi duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako