• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Zaidi ya watalii 7000 watarajiwa Lamu

    (GMT+08:00) 2018-06-22 19:23:57

    Zaidi ya watalii 7000 wanatarajiwa kuzuru eneo la Lamu Kenya katika kipindi cha ziara nyingi za watalii kinachotarajiwa kuanza mwezi Julai mwaka huu.

    Waziri wa Utalii, Biashara na Viwanda wa Kaunti ya Lamu, Dismas Mwasambu, anasema hatua hiyo inatokana na imani ambayo imerejeshwa kwa watalii hasa baada ya usalama kudhibitiwa kote Lamu.

    Sekta ya Utalii ya Lamu imekuwa ikipokea changamoto tele hasa tangu Al-Shabaab walipovamia na kuua wakazi zaidi ya 100 kwenye miji ya Mpoeketoni, Kibaoni, Witu na Hindi kati ya 2014 na 2015.

    Akizungumza wakati wa kongamano la washikadau kwenye hoteli ya Majlis eneo la Shella Alhamisi, Bw Mwasambu aliwashauri wenye mahoteli kote Lamu kujiandaa vilivyo ili kupokea watalii wengi zaidi kutoka kutoka sehemu mbalimbali za nchi na ng'ambo punde Julai itakapoanza.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako