• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Watu laki 2.4 walazimishwa kuacha kutumia dawa za kulevya nchini China

    (GMT+08:00) 2018-06-25 18:45:55

    Tarehe 26 Juni ni siku ya kimataifa ya kupiga marufuku dawa za kulevya. Naibu waziri wa sheria wa China Bw. Liu Zhiqiang leo hapa Beijing amesema, hivi sasa nchini China kuna watu laki 2.4 wanaolazimishwa kuacha kutumia dawa za kulevya.

    Ofisi ya habari ya baraza la serikali ya China leo imefanya mkutano na waandishi wa habari, ili kujulisha hali ya kuwasaidia watu kuacha kutumia dawa za kulevya. Naibu waziri wa sheria wa China Bw. Liu Zhiqiang anasema,

    "Kwa mujibu wa sheria ya kupiga marufuku dawa za kulevya na nidhamu za kuacha matumizi ya dawa hizo, idara za utekelezaji wa sheria zina majukumu ya kuwalazimisha watumiaji waache matumizi ya dawa za kulevya, na kusimamia juhudi za kuwasaidia watumiaji kuacha. Hadi sasa idara za utekelezaji wa sheria zimeanzisha vituo 361 vya kuwasaidia watu kuacha matumizi ya dawa za kulevya, ambavyo vimewasaidia watu zaidi ya milioni 1.3 tangu sheria ya kupiga marufuku ianze kutekelezwa mwaka 2008."

    Bw. Liu amesema China imekamilisha mfumo wa kuwasaidia watu kuacha matumizi ya dawa za kulevya, na ina wataalamu na wafanyakazi husika wa kutosha. Ingawa juhudi za kuwasaidia watumiaji kuacha matumizi ya dawa za kulevya zimepiga hatua dhahiri, lakini China bado inakabiliwa na changamoto kubwa haswa matumizi ya dawa za aina mpya. Mkuu wa idara ya kusimamia juhudi za kuwasaidia watumiaji kuacha matumizi ya dawa za kulevya ya wizara ya sheria ya China Bw. Cao Xuejun anasema,

    "Hivi sasa matumizi ya dawa za kulevya za aina mpya yamejitokeza. Watumiaji wa dawa hizo wanaotibiwa kwenye vituo vya kuwasaidia watu kuacha matumizi ya dawa za kulevya wanaongezeka mwaka hadi mwaka, na wanachukua asilimia 53 ya watumaiji wote."

    Bw. Cao amesema, licha ya serikali, jamii na familia za watumiaji wa dawa za kulevya, pia zinaweza kutoa mchango muhimu kwa juhudi hizo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako