• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Idara za uendeshaji wa mashtaka za China zakabiliana na uhalifu wa dawa za kulevya kwa juhudi kubwa

  (GMT+08:00) 2018-06-26 19:20:45

  Leo ni siku ya kimataifa ya kupambana na dawa za kulevya. Idara kuu ya uendeshaji wa mashtaka ya China imetoa ripoti ikisema, kuanzia mwezi Januari hadi April mwaka huu, idara za uendeshaji wa mashtaka katika ngazi mbalimbali nchini China zimeidhinisha kuwakamata watu 31,679, na kuwashtaki watu 35,193 waliotuhumiwa kuhusika na uhalifu wa dawa za kulevya, ili kudumisha shinikizo kubwa dhidi ya uhalifu huo.

  Mapambano dhidi ya dawa za kulevya hayawezi kulegalega mpaka kuwe na ushindi kabisa. Katika miaka ya hivi karibuni, idara za uendeshaji wa mashtaka katika ngazi tofauti nchini China zimeongeza nguvu ya kuadhibu uhalifu wa dawa za kulevya. Naibu mkurugenzi wa ofisi ya pili ya mashtaka ya umma ya idara kuu ya uendeshaji wa mashtaka ya China Bw. Huang Weiping anasema,

  "Kwa mujibu wa sheria husika, tunawaadhibu vikali wahalifu wa dawa za kulevya, haswa wale waliopambana na askari polisi kwa silaha, ili kudumisha shinikizo kubwa dhidi ya uhalifu wa dawa za kulevya."

  Licha ya kuwakamata na kuwashtaki wahalifu wa dawa za kulevya, idara za uendeshaji wa mashtaka za sehemu mbalimbali pia zimeimarisha usimamizi kwa upelelezi wa uhalifu wa dawa za kulevya. Mwendesha mashtaka wa ngazi ya juu wa idara kuu ya uendeshaji wa mashtaka ya China Bw. Liu Mingchao anasema,

  "Idara za kuendesha mashtaka zimefanya kazi kwa bidii kadri iwezavyo. Zinawashtaki wahalifu waliokosa, kupitia usimamizi kwa upelelezi wa polisi, na kusahihisha hukumuza mahakama zenye makosa kupitia usimamizi wa mahakama.

  Licha ya kushughulikia uhalifu wa dawa za kulevya, idara za uendeshaji wa mashtaka pia zinadadisi uwezekano wa ufisadi kwa wafanyakazi wa serikali. Kwa mfano idara ya uendeshaji wa mashtaka ya mkoa wa Sichuan iligundua naibu jaji mkuu wa mahakama akiwasaidia wahalifu wa dawa za kulevya kuepuka adhabu ya kisheria, na hatimaye alihukumiwa kifungo cha miaka 12 jela.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako