• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • EAC: Mawaziri wa Afrika Mashariki wasifu reli ya Kenya iliojengwa na China

    (GMT+08:00) 2018-06-26 19:34:05

    Mawaziri wa Afrika Mashariki wamesifu reli ya Kenya iliojengwa na China wakisema haijasaidia tu kufanya biashara kwenye kanda hiyo lakini pia ni mfano wa jinsi uwekezaji kwenye miundo mbinu unaweza kuleta mageuzi ya kiuchumi.

    Waziri wa uchukuzi na barabara wa Sudan Kusini John Luk Jok, amesema kuna maendeleo makubwa katika utekelezaji wa miundo mbinu ya ushoroba wa kaskazini lakini pia akahoji kuwa ukosefu wa fedha unasalia kuwa changamoto kubwa.

    Naye waziri wa jumuiya ya Afrika Mashariki wa Kenya Peter Munya, amesema reli ya kisasa ya SGR imepunguza muda wa kusafirisha mizigo na pia kupunguza msongamano barabarani.

    Mwaziri hao wako mjini Nairobi kwa mkutano wa siku mbili wa 14 kuhusu miradi ya ushoroba wa kaskazini unaounganisha kanda hiyo.

    Ushoroba wa kaskazini ni miundo mbinu ya kibiashara inayounganisha nchi za maziwa makuu na bandari ya Mombasa nchini Kenya.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako