• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya: Wenye benki watoa masharti mapya kwa wateja

    (GMT+08:00) 2018-06-26 19:36:36

    Wateja wa benki nchini Kenya wanaohitaji kutoa au kuweka shilingi milioni 10 watahitajika kutoa notisi ya siku tatu na kuoata idhini ya kufanya hivyo kutoka kwa mkuu wa tawi husika la benki.

    Hatua hiyo iliotangazwa na chama cha wenye benki inalenga kukabiliana na ubadhirifu wa pesa.

    Aidha wateja wanaofanya biashara kwenye benki inayozidi milioni 10 watahitajika kutoa nakala za vitambulisho au paspoti ya wale wanaowatumia pesa.

    Na pesa zozote zaidi ya shilingi milioni 20 zitahitajika kuidhinishwa na maneja wa tawi ama mkurungezi wa benki husika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako