• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China kuendelea kuimarisha ushirikiano wa aina mbalimbali katika mapambano dhidi ya dawa za kulevya

    (GMT+08:00) 2018-06-26 19:56:15

    Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang leo hapa Beijing amesema, China siku zote inazingatia kupambana na dawa za kulevya, kuunga mkono na kushiriki kwenye ushirikiano wa kimataifa wa mapambano dhidi ya dawa za kulevya.

    Amesema China pia imesaini makubaliano na nchi mbalimbali katika kupambana na dawa za kulevya, na katika siku zijazo, China itaendelea kushirikiana na nchi mbalimbali ili kujenga dunia isiyo na dawa za kulevya. China imejiunga kwenye mkataba wa Umoja wa Mataifa wa mapambano dhidi ya dawa za kulevya, kuzidisha ushirikiano na kamati ya dawa za kulevya ya umoja huo, na mashirika mengine ya kupambana na dawa za kulevya. Pia amesema China inaunga mkono na kuhimiza ushirikiano wa kikanda, na kusaidia nchi jirani kupambana na dawa za kulevya. Aidha, China inashirikiana na jumuiya ya kimataifa katika kubadilishana taarifa za kipelelezi kuhusu dawa za kulevya, mafunzo na utekelezaji wa sheria, ili kupambana kwa ufanisi dhidi ya uhalifu wa dawa za kulevya unaovuka mipaka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako