• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa nne wa Baraza la ushirikiano wa vyombo vya habari kati ya China na Afrika wafanyika Beijing

    (GMT+08:00) 2018-06-27 10:14:25

    Mkutano wa nne wa Baraza la ushirikiano wa vyombo vya habari kati ya China na Afrika umefanyika mjini Beijing, ambapo vyombo vya habari vya China na Afrika vimesaini makubaliano 12 ya ushirikiano, na kupitisha azimio kuhusu kuimarisha mawasiliano na ushirikiano.

    Mkutano huo unalenga kuunga mkono Mkutano wa kilele wa Baraza la ushirikiano kati ya China na Afrika FOCAC utakaofanyika mwezi Septemba hapa Beijing, kutekeleza makubaliano yaliyofikiwa kwenye Mkutano uliopita wa baraza hilo uliofanyika mwaka 2015 nchini Afrika Kusini, na kupanua mawasiliano na ushirikiano kati ya China na Afrika katika sekta ya vyombo vya habari.

    Kwa mujibu wa azimio la pamoja lililopitishwa kwenye mkutano huo, pande hizo mbili zimeamua kuimarisha mazungumzo ya kisera na ushirikiano katika sekta muhimu za matangazo ya habari, mipango ya habari, pia kukuza mawasiliano na ushirikiano wa vyombo vya habari katika matangazo ya masuala muhimu ya kikanda na kimataifa chini ya mfumo wa FOCAC.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako