• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Vitendo vya kujilinda kibiashara vyaanza kusababisha athari mbaya kwa Marekani yenyewe

  (GMT+08:00) 2018-06-27 17:07:11

  Kampuni ya Harley Davidson ya pikipiki ya Marekani tarehe 25 imetangaza kuhamishia baadhi ya shughuli zake nje ya Marekani, ili kuepuka ushuru wa forodha utakaotozwa na Umoja wa Ulaya dhidi ya bidhaa za Marekani. Marekani imeanza kukabiliwa na athari mbaya kutokana na vitendo vyake ya kujilinda kibiashara.

  Baada ya kampuni ya Harley Davidson kutangaza kuhamishia baadhi ya shughuli zake nje ya Marekani, soko la hisa nchini Marekani limeshuka kwa kiasi kikubwa, na thamani za kampuni tano kubwa za teknolojia za Marekani Facebook, Amazon, Apple, Netflix na Alphabet zimepungua kwa dola za kimarekani bilioni 80. Hali hii imemkasirisha sana rais Donald Trump wa Marekani, ambaye ameandika mara kadhaa kwenye Twitter akilaani kampuni ya Harley Davidson kwa kusalimu amri, na itaadhibiwa kwa kutozwa ushuru mkubwa na serikali ya Marekani hadi ifilisike.

  Rais Trump anaona kuwa kampuni ya Harley Davidson iliyomsaidia kuwa rais wa Marekani ni mwakilishi hodari wa kampuni za Marekani, na madhumuni ya serikali ya Marekani kuongeza ushuru wa forodha kwa bidhaa za nchi za nje ni kuzilinda kampuni za Marekani kama Harley Davidson, na kuzihamasisha kurudisha viwanda na mitaji nchini Marekani. Lakini sasa kitendo cha kampuni hiyo kinaenda kinyume na matarajio yake.

  Lakini sababu halisi ya kampuni ya Harley Davidson kuhamishia baadhi ya shughuli zake nje ni vitendo vya kujilinda kibiashara vya serikali ya Marekani. Umoja wa Ulaya ulitangaza kuongeza ushuru wa forodha wa pikipiki zinazotengenezwa na kampuni hiyo kuwa asilimia 31 kutoka 6, ili kulipiza kisasi vitendo vya kujilinda kibiashara vya Marekani. Baadaye bei ya pikipiki hiyo itaongezeka kwa dola za kimarekani 2,200 katika soko la Ulaya, na hali hii imelazimisha kampuni hiyo kuhamisha baadhi ya uzalishaji wake kutoka Marekani.

  Ikiwa kampuni ya kwanza ya Marekani inayohamisha baadhi ya shughuli zake kutoka nchini humo, uamuzi wa kampuni ya Harley Davidson ni alama ya kushindwa kwa sera ya biashara ya serikali ya Trump. Hivi leo kampuni za nishati, kilimo na uzalisajiezaji za Marekani zinakabiliwa na changamoto kubwa, kutokana na Umoja wa Ulaya, China, India, Uturuki, Mexico na nchi nyingine nyingi kutangaza hatua za kulipiza kisasi vitendo vya kujilinda kibiashara vya Marekani.

  Mkurugenzi wa Shirika la Fedha Duniani Bibi Christine Lagarde na katibu mkuu wa Shirika la Biashara Duniani Bw. Christian Ewert, hivi karibuni wameonya tena, "hakuna mshindi katika vita vya biashara". Wachambuzi wanaona Marekani itajitatiza kutokana na vitendo vyake vya kujilinda kibiashara.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako