• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mawaziri wa ulinzi wa China na Marekani wafanya mazungumzo

    (GMT+08:00) 2018-06-27 19:57:46

    Waziri wa ulinzi wa China Bw. Wei Fenghe leo hapa Beijing amefanya mazungumzo na mwenzake wa Marekani Bw. James Mattis.

    Bw. Wei Fenghe amesema, jeshi la China linashikilia kulinda mamlaka ya nchi, usalama na maslahi ya maendeleo ya China, na pande hizo mbili ni lazima kushikilia kutopambana, kuheshimiana, kushirikiana na kunufaishana, ili kutimiza maendeleo ya pamoja.

    Bw. Mattis amesema kuwa, maendeleo ya China yananufaisha Marekani na dunia, na kwamba nchi hizo mbili zinatakiwa kuishi kwa masikilizano. Marekani inatumai kushirikiana na China kuboresha mfumo wa mawasiliano, kuhimiza mazungumzo, na kuimarisha usimamizi wa hali ya hatari. Amesema anaamini Marekani na China zinaweza kuhimiza amani na maendeleo ya dunia kwa ushirikiano.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako