• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya:Agizo la kuchunguza mali za watumishi wa umma launga mkono

    (GMT+08:00) 2018-06-28 21:04:27
    Viongozi wa utumishi wa umma wamemtaka Rais Uhuru Kenyatta kuwachukulia hatua baadhi ya viongozi wanaokataa kuchunguzwa mali zao.

    Viongozi hao wamesema mtumishi yeyote wa umma anaekataa kuchunguza mali zake anafaa kuadhibiwa na rais ili kuimarisha vita dhidi ya ufisadi.

    Hatua hii inajiri baada ya kukithiri kwa visa vya uhalifu katika idara tofauti za umma nchini Kenya hususan sakata la hivi majuzi la ubadhirifu wa fedha za vijana na sakata la sukari.

    Watumishi wa umma wamekumbwa na kashfa za kutumia fedha za serikali bila uwajibikaji.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako