• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yafafanua utekelezaji wa ahadi zake tangu ijiunge na WTO

    (GMT+08:00) 2018-06-28 21:18:23

    Ofisi ya habari ya baraza la serikali la China leo kwa mara ya kwanza imetoa waraka wa China na Shirika la Biashara Duniani WTO, na kufafanua utekelezaji wa ahadi zake kwa Shirika hilo.

    Wachambuzi wanaona kuwa waraka huo si kama tu unawasaidia watu kufahamu mchango wa China tangu ijiunge na WTO, bali pia kuwafahamisha sababu ya China ya kushikilia utaratibu wa biashara wa pande mbalimbali.

    Hadi mwezi Agosti mwaka 2010, China ilitekeleza ahadi zake zote ilizotoa wakati ilipojiunga na WTO. Kuanzia mwaka 2001, malipo ya hakimiliki ya ujuzi ya China kwa nchi za nje yaliongezeka kwa asilimia 17 kila mwaka, na mwaka 2017 yalifikia dola za kimarekani bilioni 28.6.

    Katibu mkuu wa zamani wa WTO Bw. Pascal Lamy alisema, watu wengi wanafuatilia mauzo ya China katika nchi za nje, lakini hawajatambua kuwa China pia ni nchi inayonunua vitu vingi kutoka nchi nyingine. China imetoa mchango muhimu kwa ajili ya maendeleo ya uchumi wa dunia.

    Wachambuzi wamesema bidhaa zilizotengenezwa na China zimekidhi mahitaji ya wateja wa dunia, huku soko kubwa la China pia likivutia sana dunia nzima. China imesamehe ushuru wa forodha wa bidhaa nyingi za nchi zinazoendelea, mbali na hiyo inanufaisha nchi nyingine kwa pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja na makubaliano ya ushirikiano.

    Kutokana na sera ya ufunguaji mlango, dunia itanufaika na maendeleo ya China, nchi mbalimbali duniani zinapaswa kufuata kanuni ya WTO, na kushikilia kufungua mlango, ili kukabiliana na changamoto kwa pamoja, na kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako