• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Gimba la angani lililoingia mfumo wa jua mwaka jana huenda ni nyota mkia

    (GMT+08:00) 2018-06-29 14:16:10

    Mwaka jana darubini ya taasisi ya unajimu ya Chuo Kikuu cha Hawaii cha Marekani iligundua sayari ndogo yenye umbo la sigara. Sayari hii ilipewa jina la Oumuamua, ambalo linamaanisha "mjumbe kutoka mbali" katika lugha ya Kihawaii. Hii ni mara ya kwanza kwa binadamu kugundua sayari inayotoka nje ya mfumo wa jua, na mwishowe sayari hiyo ikaondoka.

    Lakini Utafiti mpya unaonesha kuwa gimba hili huenda ni nyota mkia badala ya sayari ndogo. Gimba hili linaondoka kutoka mfumo wa jua kwa kasi zaidi kuliko ilivyokadiriwa.

    Mnajimu wa idara ya anga ya juu ya Ulaya Marco Micheli amekadiria kuwa gimba hili huenda ni nyota mkia, baada ya kupashwa moto na jua, nyota mkia itatoa vitu na kupata msukumo mkubwa zaidi, na kuifanya iondoke kwa kasi zaidi.

    Mnajimu wa Chuo Kikuu cha Hawaii Karen Meech amesema uchunguzi unaonesha kuwa nyota mkia huenda inatoa vumbi kubwa sana.

    Watafiti wamesema bado hawajui mambo mengi kuhusu gimba hili, kwa mfano, linatoka wapi

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako