• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uhasama wa kibiashara watajwa kuwa chanzo cha moto uliosababisha vifo vya watu 15

    (GMT+08:00) 2018-06-29 18:50:05

    Mivutano kuhusu ardhi na ushindani wa kibiashara ndizo sababu kuu zinazodaiwa kupelekea vifo vya watu 15 kwenye moto uliotokea katika soko la Gikomba, Nairobi usiku wa kuamkia Alhamisi.

    Tukio hilo ndilo baya zaidi kuwahi kusababisha maafa makubwa kwenye misururu ya moto ambayo huzuka katika soko hilo maarufu mara kwa mara. Kwenye visa vya awali, mali ya thamani kubwa imekuwa ikiharibiwa, lakini kwenye moto huo maisha ya wengi yaliangamia.

    Wengi wa waathiriwa hao walifariki wakiwa majumbani mwao, kwani walikuwa wangali wamelala.

    Mengi ya makazi yaliyo karibu yalikuwa yamechomeka kabisa, yakionyesha ukubwa wa moto huo.Wafanyabiashara na wakazi wa mitaa inayopakana na soko hilo walielezea kwamba kumekuwa na taharuki za ushindani wa kibiashara katika soko hilo. Baadhi ya wafanyabiashara wanaamini kwamba walinzi wao walitumika kimakusudi na mahasimu wao kuwasha moto huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako