• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Ofisa wa ngazi ya juu wa CPC akutana na waziri wa usalama wa ndani wa Afrika Kusini

    (GMT+08:00) 2018-06-29 19:14:54

    Mjumbe wa Ofisi ya siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) Yang Jiechi amekutana na Waziri wa Ulinzi wa Afrika Kusini Dipuo Letsatsi-Duba mjini Durban.

    Katika mazungumzo yao, Bi. Letsatsi-Duba amesema Afrika Kusini inaipongeza China kwa kuiunga mkono na nafasi yake muhimu katika kushughulika na masuala ya Afrika. Amesema Afrika Kusini inapenda kutumia kumbukumbu ya miaka 20 ya kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia kama fursa ya kuongeza ushirikiano wa kina wa kunufaishana kati ya nchi hizo mbili.

    Naye Bw. Yang Jiechi amesema, huu ukiwa ni mwaka wa 20 wa kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili, uhusiano kati ya China na Afrika Kusini unakabiliwa na fursa muhimu za maendeleo. Amesema China inaunga mkono Afrika Kusini kuwa mwenyeji wa mkutano wa 10 wa kilele wa BRICS, ambao rais Xi Jinping wa China anatarajiwa kuhudhuria.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako