• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Jumuiya ya kimataifa yasifu mtazamo wa CPC kuhusu kushughulikia mambo ya dunia nzima

    (GMT+08:00) 2018-07-01 19:56:19

    Wakati wa maadhimisho ya miaka 97 ya kuanzishwa kwa Chama cha kikomunisit cha China, baadhi ya wajumbe wa vyama vya nchi za nje wamesema, chama cha kikomunisti cha China kinaongoza China kushikilia mtazamo wa kujadiliana kwa pamoja, kujenga kwa pamoja na kunufaika kwa pamoja katika kushughulikia mambo ya dunia nzima, kuhimiza kujenga uhusiano wa aina mpya wa kimataifa, kusukuma mbele kujenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa binadamu, kufanya umuhimu wake katika mambo ya kimataifa, na kutoa busara na nguvu zake wa ajili ya mageuzi na ujenzi wa mfumo wa kushughulikia mambo ya dunia nzima.

    Naibu katibu wa kamati kuu ya chama tawala cha Russia Sergei Zheleznyak amesema kuwa, pendekezo la China la kujenga jumuiya ya mustakabali wa pamoja wa binadamu ni pendekezo lenye busara, nchi mbalimbali zinapojenga jumuiya yenye mustakabali wa pamoja wa binadamu hakika watabeba wajibu wao wa kuhimiza maendeleo ya ustaarabu wa binadamu, kuendeleza uhusiano kwenye msingi wa kufanya ushirikiano wa kunufaishana ili kupata maendeleo kwa pamoja, hayo yanasaidia amani na maendeleo ya dunia. Russia inapenda kushirikiana na China kuhimiza utekelezaji wa pendekezo hilo.

    Katibu mkuu wa chama cha kikomunisti cha Uingereza Bw. Robert Griffiths anaona kuwa, chama cha kikomunisti cha China kinashikilia kuzingatia binadamu, kuweka mkakati wake wa maendeleo kwa hali yake yenyewe na mahitaji yake, na kupata mendeleo katika kujenga nchi za kisasa za kisosiolisti, hayo yana umuhimu mkubwa wa kuigwa kwa dunia. Chama cha kikomunisti cha China kinaongoza China kuondoa watu maskini zaidi milioni 700, na kutoa mchango mkubwa katika mambo ya kuondoa umaskini duniani.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako