• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kikapu, Kufuzu kombe la dunia: Rwanda yafuzu raundi ya pili, Uganda yashindwa

    (GMT+08:00) 2018-07-02 10:51:37

    Timu ya taifa ya Rwanda imefuzu kwa hatua inayofuata ya mechi za kufuzu michuano ya kombe la dunia ya mchezo wa mpira wa kikapu itakayofanyika nchini China mwaka 2019.

    Rwanda imefuzu baada ya kushinda kwa alama 92-79 kwenye mechi ya mwisho ya raundi ya pili ya hatua ya makundi iliyofanyika jana mjini Lagos nchini Nigeria.

    Kwa kufuzu, Timu hiyo sasa ambayo iko nafasi ya pili kwenye msimamo wa kundi lake inaungana na timu za Nigeria ambayo inaongoza, pamoja na Mali iliyoshika nafasi ya tatu, na Uganda ikiwa ni timu pekee iliyoshindwa kufuzu katika kundi hilo.

    Kwa kufuzu hatua inayofuata, Rwanda sasa imepangwa kundi F la kanda ya Afrika pamoja na timu za Senegal, Nigeria, Jamhuri ya Afrika ya Kati, Ivory Coast na Mali.

    Na mechi kwa ajili ya kufuzu za kundi hilo la mwisho zitapigwa mwezi Septemba mwaka huu ikiwa ni raundi ya kwanza na Februari mwakani ikiwa ni raundi ya pili.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako