• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mkutano wa 31 wa viongozi wa Umoja wa Afrika waanza

    (GMT+08:00) 2018-07-02 11:08:48

    Mkutano wa 31 wa viongozi wa Umoja wa Afrika umeanza huko Nouakchott nchini Mauritania.

    Katika mkutano huo wa siku mbili wenye kauli mbiu ya "kupambana na ufisadi: njia endelevu ya mageuzi ya Afrika", viongozi wa nchi mbalimbali watafanya majadiliano kuhusu mageuzi ya Umoja wa Afrika, eneo la biashara huria la Afrika, vita dhidi ya ufisadi na ugaidi na usalama wa kikanda.

    Rais Mohamed Ould Abdel Aziz wa Mauritania jana katika ufunguzi wa mkutano huo alisema kuwa ushindi dhidi ya ufisadi ni msingi wa maendeleo ya bara la Afrika, na kupambana na ufisadi kutasaidia kutoa fedha kwa ajili ya miradi muhimu kwa nchi za Afrika hasa katika sekta ya nishati, mawasiliano na miundo mbinu. Pia amesema pande zote zinapaswa kufikia makubaliano chini ya utaratibu wa Umoja wa Afrika kuhusu kukabiliana na matishio yanayozuia maendeleo endelevu ya Afrika ikiwemo ufisadi, dawa za kulevya na msimamo mkali.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako