• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Kwanini binadamu wanachunguza sayari ndogo

  (GMT+08:00) 2018-07-02 14:12:28

  Sayari ndogo ni magimba madogo ulimwenguni, lakini hivi karibuni zimefuatiliwa sana na binadamu. Chombo cha uchunguzi cha Hayabusa 2 cha Japan kimefika sayari ndogo ya Ryugu tarehe 27, na chombo cha uchunguzi wa OSIRIS-REx cha Marekani kitafika sayari ndogo ya Bennu mwezi Agosti.

  Mwanzoni mwa mwaka huu, jarida la Nature la Uingereza limeweka uchunguzi wa sayari ndogo kuwa matukio ya kisayansi yanayostahili kufuatiliwa mwaka huu. Je, kwanini binadamu wanachunguza sayari ndogo? Mtafiti wa kituo cha uchunguzi wa anga ya juu cha Taasisi ya sayansi ya China Dr. Zheng Yongchun amesema binadamu wana sababu tatu za kufanya uchunguzi wa sayari ndogo.

  Kwanza, uchunguzi wa sayari ndogo unasaidia kuelewa chimbuko na mabadiliko ya mfumo wa jua. Sayari ndogo hazibadilikibadiliki mara kwa mara kutokana na sababu za kijiolojia kama dunia, na vitu vilivyokuwepo wakati mfumo wa jua ulipoundwa vinahifadhiwa vizuri zaidi kwenye sayari hizi.

  Pili, uchunguzi huo unasaidia kuepusha hatari ya sayari ndogo kugonga dunia. Wanasayansi wengi wamekubali kuwa dinosaur walitoweka duniani kutokoana na mgongano wa sayari ndogo katika miaka milioni 65 iliyopita. Binadamu wanatakiwa kufahamu mizingo ya sayari ndogo, na kutafiti njia ya kuepusha mgongano wa sayari hizi.

  Tatu, Sayari ndogo huenda zina thamani kubwa ya kiuchumi. Baadhi ya sayari ndogo zina madini yasiyokuwepo kwa wingi duniani, na siku hizi baadhi ya makampuni yameanzisha utafiti kuhusu teknolojia ya kuchimba madini kwenye sayari ndogo.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako