• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda: Waganda wanapanga kuhepa malipo ya mitandao ya kijamii

    (GMT+08:00) 2018-07-02 19:43:47

    Uganda inapanga njia za kuepuka kodi ya mtandao ya kijamii ambayo malipo yake yalianza rasmi jana.

    Kwa mujibu wa utafiti wa mitandao ya kijamii uliofanywa na gazeti la Daily Monitor, idadi kubwa ya watu waliamua kutumia mtandao wa kibinafsi Virtual Private Network (VPN) ili kuepuka kulipa malipo ya ushuru ya kila siku.

    Kulingana na matokeo ya utafiti, asilimia 19 ya wafuasi 581 ambao walishiriki katika utafiti huo, wamesema watatumia muda mdogo kwenye mitandao ya kijamii , asilimia 11 wamesema wataacha kutumia mitandao ya kijamii, wakati asilimia 70 wamesema watatumia VPN.

    Kodi mpya ambayo itatonzwa kila siku kwa mganda yeyote anatumia jukwaa la mtandao ya kijamii atalipa dola 0.05 (Shs200) kila siku, dola 0.36 (Shs1, 400) kila wiki au dola 1, 56 (Shs 6,000) kila mwezi kama ushuru.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako