• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • LIANG JIA HE 5

    (GMT+08:00) 2018-07-02 19:51:53

    "Njoo, mtoto, ingia ndani ingia!" Ndani ya nyumba ya mapango ya mlima, vijana wasomi walimwita kwa sauti ndogo mtoto Wu Hui aliyesima nje ya mlango.

    Wu Hui alikuwa bado anasimama tu, ambaye alivaa nguo kukuu iliyoraruka kweli hajui kusema nini. Kihalisi yeye si mtoto tena, ila ni mwembamba na anaonekana kama ni mdogo.

    Mwaka ule, Wu Hui alikuwa na miaka 14, ni mdogo kwa mwaka mmoja kuliko Xi Jinping, kabla ya vijana wasomi kufika kijijini kwao kutoka Beijing alirudi Liang Jiahe kutoka sekondari siku chache tu.

    Wakati huo ni siku za baridi, vijana wasomi walikuwa hawajui namna ya kuchoma moto ili kitanda chao cha udongo kitapashwa joto, amba sivyo ndani ya pango la mlima ni baridi sana, hivyo wakamwuliza Wu Hui aliyesimama nje ya mlango anajua kuchoma moto au la, Wu Hui alisema: "Hakika najua." Katika vijiji watu wote wanajua kuchoma moto kitanda cha udongo, pamoja na watoto, Wu Hui aliingia nyumba yao akionekana ana hofu kidogo.

    Ndiyo hiyo, Wu Hui alikuwa mgeni aliiyekuja mara kwa mara katika nyumba za mapango ya mlimani. Wu Hui ni mfupi, lakini ni mwenye akili zaidi. Yeye alifurai kuwasaidia vijana wasomi kuondoa kizuizi cha lugha kati yao na wanakijiji, kwani aliposoma shuleni alijua kuongea kwa lugha ya Beijing, kama vijana wasomi hawaelewi kilugha cha Yanchuan wakamwuliza yeye, hivyo yeye alikuwa kama mtafsiri wao.

    Ameitwa kuwa mtafsiri wa vijana wasomi, hivyo kila mara alikuwa kwao, mbali na kupenda kupiga soga nao, alivutiwa sana na vitabu vilivyosomwa na vijana wasomi. Aliposoma shuleni mbali na vitabu vya shuleni, hakuwahi kupata vitabu vingine, hata hakuwahi kuona kitabu kicho nene, alipokuwa kwao, alipekuapekua na kusomasoma, vijana wasomi waliona anapenda kusoma walimwambia kama anapenda anaweza kuchukua kusoma nyumbani.

    Kitabu cha kwanza alikiazima kutoka kwa Xi Jinping kitwacho "Maswali Laki moja", alifikiri kama nimeelewa maswali laki moja nitakuwa mtu mwenye ujuzi na hodari, alifurahi saa.

    Kitabu hiki kweli kilimfungulia dirisha moja la dunia yenye ujuzi mwingi usio na upeo. Alisoma sana hata alipoona njaa alikula donge lenye makapi huku akisoma na kuona donge hili ni rahisi kumeza.

    Baadaye alizima vitabu vingine kadha wa kadha kutoka kwa Xi Jinping, akaanza kuwasiliana kiroho na vijana wasomi. Alihisia tabia wazi na udhati kutoka kwa Wang Yansheng na Lei Pingsheng, na kuhisia hali ya kukuwa na makuu hata kidogo na kufuata hali halisi kutoka kwa Xi Jinping. Wu Hui alisema: "Mimi ninawapenda na kuwasifu kweli, kaka hao ni mifano ya kuigwa katika maisha yangu."

    Chini ya ushawishi wa Xi Jinping, Wu Hui alisoma vitabu na kuimaarisha nia ya kuendelea kusoma katika chuo kikuu. Mwaka 1973 alikwenda kushiriki mtihani na kuandikishwa na chuo cha ualimu cha Yan'an. Alipokwenda chuoni Xi Jinping alimzawadia vitu na nguo, na alipohitimu masomo, Xi Jinping aliondoka Liang Jia He. Wu Hui alifanya kazi ya ualimu katika shule moja moja, baadaye akawa ofisa shuleni, lakini bila kujali akifanya kazi gani, anafuata kwa makini kanuni yake mwenyewe yaani kutosema sana ila kutenda zaidi, ni lazima awe mtendaji hodari halisi.

    Xi Jinping alijaribu kushiriki  kwenye mtihani wa kujiunga chuo kikuu, kwani kusoma lilikuwa ni tumaini lake kubwa zaidi. Yeye na mwenzake Wu Hui walikwenda wilayani kushiriki mtihani, Xi Jinping alitarajia kuandikishwa na Chuo Kikuu cha Qinghua, lakini baadaye alikataliwa kabisa, kwani baba yake alihusika na kesi ya kubambikiwa.

    Mwaka 1975, Chuo Kikuu cha Qinghua kilitoa nafasi mbili kwa Yanchuan, Xi Jinping alipata tena fursa ya kujiandikisha, na alitimiza matumaini yake ya tatu ya kusoma Chuo kikuu cha Qinghua.

    Lakini wakati ule kulikuwa na ukaguzi wa kisiasa, wahusika walikuwa mashaka kama wamkubalie Xi kusoma katika Chuo Kikuu cha Qinghua. Wakati huo baba yake mzazi Xi Zhonxun alifanya kazi katika kiwanda kimoja cha Luoyang, kiwanda hiki kilitoa hati inayosema, ndugu Xi Zhonxun hakufanya uhalifu, mtoto wake asizuiwe kujiunga na chuo kikuu. Na Xi Jinping akaandikishwa kusoma Chuo kikuu cha Qinghua.

    Siku za kufunguliwa chuo kikuu zilikribia, lakini Xi Jinping alikuwa bado anashughulikia mambo ya Liang Jia He. Aliitisha mkutano wa kuchagua katibu wa tawi la Chama, ambapo alimpendekeza Shi Chunming, kwani aliona yeye ataweza kuwa kiongozi mzuri wa kuutumia umma, na alimwambia Shi ni lazima awe mfano wa kuigwa katika kuhimiza maendeleo ya Liang Jia He.

    Tarehe 7 Oktoba,1975 ilikuwa siku ya kuondoka Liang Jia He kwa Xi Jinping. Usiku wa siku ya juzi ya siku hiyo, Xi alipiga soga na wanakijiji mpaka usiku wa manane, asubuhi ya siku ya pili alichelewa kuamka. Alipoamka na kufungua mlango, aliona kwenye ua na kando njia wamesimama watu wengi, watu wazima, watoto, na wazee, watu wote wa kijiji hicho walikuja, na mikononi mwa walishika zawadi za mazao ya kilimo kwa ajili yake, na walisimama kimyakimya. Mara Xi Jinping alitokwa na machozi, hii ni mara ya kwanza kwake kutokwa machozi mbele ya watu wote.

    Siku hiyo, watu wote kijijini hawakwenda mlimani kufanya kazi, walisimama kwenye foleni kumsindikiza Xi Jinping, wakamsindikiza umbali wa maili zaidi ya kumi, na vijana wenzake wa utotoni 12 walitembea kwa miguu kwa maili zaidi ya 40 wakamsindikiza mpaka mji wa Wilaya Yanchuan.

    Kwake Xi Jinping, Liang Jia He kilikuwa ni kituo cha kujiendeleza katika maisha yake, alisema: "nilikanyaga kwenye ardhi, kukaa miongoni mwa watu, nilituliza moyo, na kuona nguvu kubwa."
    Alisema: "Nilifika hapo nilipokuwa na miaka 15, nilikuwa na mashaka na kuhangaika; niliondoka hapo nilipokuwa na miaka 22, nimekuwa na malengo yangu na imani thabiti. Nitafanya mambo hali kwa ajili ya umma!"
    Alisema: "mwaka ule, mimi niliondoka huko, lakini niliacha moyo wangu huko."   

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako