• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • China yapenda kuimarisha ushirikiano wa kimataifa kuhusu utawala wa sheria

    (GMT+08:00) 2018-07-03 19:05:52

    Mkutano wa Baraza la Kimataifa la "Ukanda Mmoja, Njia Moja" kuhusu utawala wa sheria umefanyika mjini Beijing, na kutangaza Taarifa ya pamoja ya mwenyekiti.

    Msemaji wa Wizara ya mambo ya nje ya China Bw. Lu Kang amesema, taarifa hiyo inasisitiza ushirikiano kuhusu utawala wa sheria unapaswa kufanyika kwenye msingi wa majadiliano ya pamoja, mchango wa pamoja na kunufaika kwa pamoja, na kuzuia na kutatua ipasavyo migogoro, ili kuweka msingi imara wa kisheria kwa ajili ya pendekezo la "Ukanda Mmoja, Njia Moja".

    Bw. Lu Kang pia amesema China inapenda kushirikiana na pande zote, kuimarisha ushirikiano katika nyanja mbalimbali ikiwemo utawala wa sheria, ili kuhimiza ujenzi wa "Ukanda mmoja, Njia moja" upate maendeleo makubwa zaidi.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako