• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kenya-Wakulima wa kahawa kunufaika na mbolea ya bei nafuu

    (GMT+08:00) 2018-07-04 20:08:49

    Wakulima wa kahawa nchini Kenya wanatarajiwa kunufaika kwa mbolea ya bei rahisi ya kiasi cha Sh1.5bn ili kupunguza gharama ya fedha wanazotumia kununulia pembejeo.

    Hatua hiyo pia inalenga kuimarisha faida wanayopata kutokana na zao la kahawa.

    Naibu Rais William Ruto alisema kwamba fedha hizo zitatolewa kwa wakulima katika mwaka huu wa kifedha,sawa na walivyofanyiwa wakulima wa mahindi.

    Ruto alisema walichukua hatua hiyo ili kupunguza gharama ambayo wakulima wanapata katika shughuli za kilimo cha zao hilo.

    Alisema kuna haja ya kuwasaidia ili kuhakikisha wamepata faida kutokanba na mauzo ya mazao yao.

    Fauka ya hayo aliomba uwajibikaji katika matumizi ya fedha hizo ili kuhakikisha kwamba wakulima wamenufaika.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako