• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mwekezaji kutoka China kujenga kiwanda kikubwa cha dawa Tanzania

    (GMT+08:00) 2018-07-04 20:09:20

    Mwekezaji kutoka China anatarajia kujenga kiwanda cha dawa nchini Tanzania kwa thamani ya Sh.45bn ambacho kitakapokamilika kitasaidia kupunguza vifo vya watoto chini ya miaka mitano nchini humo.

    Kiwanda hicho kitazalisha sindano za Artesun za kupambana na malaria kali miongoni mwa dawa na vifaa tiba vyake.

    Hayo yalisemwa jana katika kikao kilichofanyika katika Kituo cha uwekezaji (TIC) na kuwahusisha wawekezaji ambao ni kampuni kubwa ya Fosunpharma ,Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia ,Wazee na Watoto,Ummy Mwalimu ,Waziri wa Viwanda na Uwekezaji ,Charles Mwijage na Mkurugenzi Mtendaji wa TIC,Geoffrey Mwambe.

    Waziri Ummy alisema kiwanda hicho kinajengwa na kampuni hiyo ambayo ni moja ya kampuni tatu kubwa za dawa nchini China.

    Alisema sindano ya Artesun itakayozalishwa Tanzania na kampuni hiyo itaweza kuuzwa Kenya,Uganda,Afrika Kusini,Zimbabwe na Malawi.

    Waziri Mwijage alisema kampuni ya FosunPharma ni nguli duniani ambapo kipato chao cha mwaka kinalingana na bajeti ya kuendesha nchi kwa mwaka.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako