• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania-Halotel yaondoa gharama za kutuma pesa

    (GMT+08:00) 2018-07-04 20:10:06

    Kampuni ya mawasiliano ya simu ya Halotel imeondoa gharama za kutuma pesa kwa wateja wanaotumia huduma ya kifedha ya Halopesa.

    Taarifa iliyotolewa jana kwa vyombo vya habari na Halotel ilisema hivi sasa wateja wataweza kutuma pesa bure Halopesa kwenda Halopesa ,huku pia ikipunguza gharama za kutuma fedha kutoka Halopesa kwenda mitandao mingine.

    Kuondolewa kwa makato hayo kumetafsiriwa na kampuni kama njia pekee ya kupanua wigo wa huduma za kifedha kwa mamilioni ya watanzania ambao wanatumia huduma za kifedha kwa njia ya simu.

    Aidha,taarifa hiyo ilisema mkurugenzi wa Kitengo cha Halopesa,Vu Tuan Long,alisema kuondolewa kwa gharama hizo kutawezesha wateja wa mtandao huo,hasa walioko maeneo ya vijijini kufanya miamala ya simu na kuondokana na usumbufu ambao wangeweza kupata kwa kutumia njia nyingine kutuma fedha ili kuokoa gharama za makato ya kufanya miamala.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako