• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Rais wa China asisitiza kuweka kipaumbele kwenye utekelezaji wa mkakati wa kustawisha vijiji

    (GMT+08:00) 2018-07-05 19:02:20

    Rais Xi Jinping wa China amesisitiza kuwa utekelezaji wa mkakati wa kustawisha vijiji ni mpango muhimu uliotolewa katika mkutano mkuu wa 19 wa chama cha Kikomunisti cha China, CPC.

    Rais Xi amesema mpango huo pia ni kipaumbele cha kazi kuhusu wakulima, kilimo na vijiji, hivyo idara za sehemu mbalimbali zinatakiwa kuelewa maana kubwa ya kutekeleza mkakati huo na kuuweka utekelezaji huo kwenye hadhi ya juu.

    Rais Xi amesema hayo kwenye mkutano wa kuhimiza kazi ya mkakati wa kustawisha vijiji uliofanyika hapa Beijing.

    Wakati huohuo, mkutano wa 8 wa mawaziri wa baraza la ushirikiano kati ya China na nchi za kiarabu utafanyika Julai 10 hapa Beijing, rais Xi Jinping anatarajiwa kuhudhuria na kuhutubia ufunguzi wa mkutano huo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako