• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Tanzania:Nyumba za barabara ya kinondoni kubomolewa

    (GMT+08:00) 2018-07-05 20:12:40

    MKUU wa Wilaya ya Kinondoni, Ally Hapi ametoa mwezi mmoja kwa watu waliojenga kwenye hifadhi za barabara kubomoa majengo yao.

    Aidha amewataka wahandisi na Wakala wa Barabara Mijini na Vijijini (TARURA) Kinondoni kufanya uhakiki maeneo yote ya hifadhi ya barabara yaliyoendelezwa kinyume na taratabu ili yabomolewe.

    Ameagiza wale waliojenga maghorofa kinyume na vibali walivyopewa wabomoe majengo yao pekee yao kabla Halmashauri haijafanya hivyo. Hapi alitoa maagizo hayo jana wakati akizungumza na waandishi wa habari baada ya kutembelea maeneo mbalimbali ikiwemo Masaki, Oysterbay na Mikocheni ambapo alibaini watu wengi kumiliki maeneo ya hifadhi ya barabara kinyume na utaratibu.

    Aliongeza kuwa watu wengi wamejenga kuta kubwa katika hifadhi za barabara, jambo ambalo ni tabu kwa watembea kwa miguu na watumiaji wa magari ambao wakipata dharura hawatakuwa na maeneo ya kusimama kwa ajili ya kushughulikia dharura zao. "Naagiza kuanzia leo Wahandisi Tarura piteni katika maeneo haya na ramani nadhani mnajua hifadhi ya barabara ni kiasi gani, fanyeni uhakiki katika maeneo yote ya hifadhi za barabara na wale waliojenga katika maeneo hayo yote yabomolewe ndani ya mwezi mmoja," alisema Hapi.

    Pia amewapa wiki moja wale waliosema wana vibali kutoka jiji kuwasilisha vibali hivyo kwa uhakiki na endapo watashindwa kufanya hivyo hatua zitachukuliwa

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako