• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Uganda:Baraza la Biashara la Afrika Mashariki lina wasiwasi kuhusu kushuka kwa biashara EAC

    (GMT+08:00) 2018-07-05 20:13:03

    Viongozi wa biashara Afrika Mashariki wametoa sauti yao kuhusu kushuka kwa biashara katika ukanda wa Afrika Mashariki,huku wengine wakisema kuwa jambo hilo sio zuri kwa ajenda ya ushirikiano wa jumuiya hiyo.

    Mwenyekiti mpya wa Baraza la Biashara Afrika Mashariki (EABC),Nicholas Nesbitt amesema biashara miongoni mwa nchi za jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) imeshuka kwa asilimia 10.1 kati ya mwaka 2013 na 2014,na kushuka zaidi,kwa asilimia 14.6 kati ya mwaka 2015 na 2016.

    Kushuka kwa biashara ya kikanda kumechangiwa pakubwa na vikwazo vya ushuru ambavyo ukanda huu wa Afrika Mashariki umekuwa ukipambana navyo kwa muda mrefu sasa.

    Aidha Nesbitt alilaumu vikwazo vya uagizaji na usafirishaji wa baadhi ya bidhaa miongoni mwa nchi wanachama.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako