• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Wizara ya Biashara ya China yasema Marekani imeanzisha vita kubwa zaidi ya kibiashara katika historia ya kiuchumi

    (GMT+08:00) 2018-07-06 13:04:18

    Wizara ya Biashara ya China imesema Marekani imeanzisha vita kubwa zaidi ya kibiashara katika historia ya kiuchumi baada ya kuanza rasmi leo kuongeza ushuru wa asilimia 25 dhidi ya bidhaa za China zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 34.

    Wizara hiyo imesema kitendo hicho cha Marekani kimekiuka kanuni za Shirika la Biashara Duniani WTO, kuathiri vibaya usalama wa mnyororo wa viwanda na mnyororo wa thamani duniani, kuzuia kufufuka kwa uchumi wa dunia, kusababisha soko la kimataifa kuyumba. Pia kitazitia hasara kampuni za kimataifa zisizo na hatia, kampuni za kawaida na wateja wa kawaida, zikiwemo kampuni za Marekani na Wamarekani.

    Wizara hiyo imeongeza kuwa China haina budi kujibu kitendo hicho ili kulinda maslahi makuu ya taifa na wananchi wake. China itatoa ripoti kwa WTO kwa wakati na kushirikiana na nchi mbalimbali duniani kulinda biashara huria na mfumo wa pande nyingi. China itashikilia kuimarisha mageuzi, kupanua ufunguaji mlango, kulinda moyo wa wajasiriamali, kuimarisha ulinzi wa hakimiliki za ubunifu na kutoa mazingira mazuri ya kibiashara kwa kampuni za nchi mbalimbali nchini China. China pia itatathmini athari zitakazopata kampuni husika na kuchukua hatua kuzisaidia.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako