• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Mtaalamu wa China asema viwanda vya matengenezo vya China havitazusha ushindani mbaya

    (GMT+08:00) 2018-07-06 17:24:09

    Mkurugenzi wa heshima wa Kamati ya wataalamu ya Shirikisho la viwanda vya mashine ya China Bw. Zhu Sendi amesema, viwanda vya uzalishaji vya China vinapaswa kubadilisha njia ya kupata maendeleo ya kutafuta ukubwa na kasi ya kupata maendeleo, kuwa kutafuta ubora na ufanisi mkubwa, na kutafuta maendeleo yenye ubora badala ya kutafuta maendeleo kwa mwendo kasi.

    Katika miaka ya hivi karibuni, viwanda vya uzalishaji vya China vimepata maendeleo kwa kasi, na ukubwa wa viwanda unachukua nafasi za mwanzo duniani, lakini bado kuna pengo kubwa kati ya China na nchi nyingine zenye uwezo mkubwa wa uzalishaji katika faida, ufanisi, ubora, muundo wa viwanda, maendeleo endelevu na matumizi ya maliasili. Bw. Zhu Sendi akizungumzia hali hiyo anasema:

    "Katika miaka kadhaa iliyopita, takwimu nyingi zimeonesha kuwa thamani ya mabehewa kadhaa ya nguo na viatu inaweza kulingana na thamani ya ndege moja ya aina ya Boeing 737, lakini hali hiyo haiwezi kudumishwa kwenye viwanda vya uzalishaji vya China, na inapaswa kutafutwa njia ya kupunguza matumizi ya nishati, na kuongeza ufanisi wa uzalishaji, ili kupata maendeleo endelevu."

    Bw. Zhu Sendi amesema, mchakato huo haumaanishi kuwa kutakuwa na ushindani mbaya kati ya China na nchi zilizoendelea katika sekta ya uzalishaji. Anasema:

    "Bila shaka tutakuwa na uhusiano wenye ushindani katika nyanja fulani, lakini mengi zaidi yatakuwa ni kukamilishana. Ingawa kutakuwa na ushindani lakini ushindani sio jambo baya ambalo pia litahimiza maendeleo."

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako