• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Waziri wa mambo ya nje wa China aeleza misimamo ya China kuhusu suala la nyuklia la Iran

  (GMT+08:00) 2018-07-07 11:00:03
  Waziri wa mambo ya nje wa China aeleza misimamo ya China kuhusu suala la nyuklia la Iran

  Mjumbe wa taifa ambaye pia ni waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi amesema, China inashikilia misimamo mitano juu ya suala la nyuklia la Iran, na inafanya juhudi kulinda na kutekeleza makubaliano ya pande zote kuhusu suala hilo, na pia italinda kithabiti maslahi halali ya China.

  Baada ya kuhudhuria mkutano wa mawaziri wa mambo ya nje kuhusu suala la nyuklia la Iran huko Vienna, Bw. Wang Yi amewaambia wanahabari misimamo hiyo mitano ni pamoja na, ni lazima kufuata kanuni za kimataifa, kutekeleza makubaliano ya pande zote, ni lazima kulinda utulivu wa Mashariki ya Kati, kuacha utiliaji vikwazo kwa upande mmoja, na kushikilia mazungumzo na mashauriano.

  Wakati huo huo, Mawaziri wa mambo ya nje wa China, Russia, Ufaransa, Uingereza, Ujerumani na Iran wamekutana mjini Vienna Ijumaa kujadili namna ya kunusuru makubaliano ya pamoja yaliyofikiwa baada ya Marekani kujitoa.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako