• Idhaa ya Kiswahili
 • Uchumi
 • Michezo
 • Facebook
 • ChinaABC
 • Sayansi
 • Afya
 • Shughuli za kubadilishana utamaduni zaboresha uhusiano kati ya China na Rwanda

  (GMT+08:00) 2018-07-08 15:51:00

  Shughuli kadhaa zinazolenga kuimarisha mabadilishano ya utamaduni na ushirikiano wa vyombo vya habari kati ya China na Rwanda na pia kuboresha uhusiano wa pande mbili zimemalizika jana mjini Kigali, Rwanda.

  Mfuko wa MW wa Beijing na Shirika la Uchapishaji la China, ambayo ni mashirika tanzu ya Kundi la Kimataifa la Uchapishaji la China kwa kushirikiana na kampuni za China zilifanya hafla ya kukusanya michango, ambapo wanafunzi 500 wa shule nchini Rwanda walipewa mabegi ya shule na taa zinazotumia umeme wa jua.

  Mkurugenzi wa Bodi ya Elimu ya Rwanda Irenee Ndayambaje amewapongeza watu wa China kwa kuendelea kuunga mkono elimu bora nchini humo. Naye naibu waziri wa Ofisi ya Habari ya Baraza la Serikali la China Guo Weimin, amewataka wanafunzi kutilia mkazo masomo na kuchangia katika maendeleo ya Rwanda katika siku zijazo. Amesema Ofisi hiyo itaendeleza miradi kama hiyo na kuunga mkono watu wa Rwanda.

  Webradio
  Sauti
  6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 1
  12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 2
  20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
  • FM 3A
  • FM 3B
  Maoni yako