• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Kombe la Kagame: Simba, Gor Mahia zatinga nusu fainali

    (GMT+08:00) 2018-07-09 10:37:23

    Simba imefanikiwa kufuzu hatua ya nusu fainali ya michuano ya kombe la Kagame inayoendelea mjini Dar es Salaam baada ya ushindi wa bao 1-0 ilipocheza dhidi ya AS Ports ya Djibouti kwenye mechi ya robo fainali.

    Goli hilo la Simba lilifungwa na mshambuliaji wake mpya, Mohammed Rashid, na timu hiyo sasa itakutana na mshindi kati ya Singida United na JKU zitakazomenyana leo.

    Kwingineko Gor Mahia ya Kenya imefuzu kwa nusu fainali baada ya kuitoa Vipers ya Uganda kwa kuifunga magoli 2-1 jana na katika mchezo wa nusu fainali itasubiri mshindi kati ya Azam FC na Rayon Sport ambazo zinashindana leo.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako