• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Waziri mkuu wa China awasili Ujerumani kwa ziara rasmi

    (GMT+08:00) 2018-07-09 10:37:50

    Kutokana na mwaliko wa chansela wa Ujerumani Bibi Angela Merkel, waziri mkuu wa China Bw. Li Keqiang amewasili Ujerumani kwa ajili ya kuhudhuria raundi ya tano ya mazungumzo kati ya serikali za China na Ujerumani na kufanya ziara rasmi.

    Bw. Li amesema nchi hizo mbili zinapaswa kusimama katika mwanzo mpya kujadili mpango wa ushirikiano wa China na Ujerumani katika siku zijazo, ili kuwanufaisha watu wa nchi hizo mbili, kuongeza nguvu ya kukuza ushirikiano kati ya China na nchi za Ulaya, na kutoa mchango katika kulinda biashara huria, mfumo wa pande nyingi na utaratibu wa kimataifa ulio wa haki na usawa.

    Wakati wa ziara hiyo Bw. Li atafanya mazungumzo na Bibi Merkel, kukutana na waandishi wa habari, kushuhudia kusainiwa kwa makubaliano ya ushirikiano kati ya China na Ujerumani, kuhudhuria Baraza la Ushirikiano wa Uchumi na Ufundi kati ya China na Ujerumani Pia Bw. Li atakutana na Rais wa Ujerumani Bw. Frank-Walter Steinmeier.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako