• Idhaa ya Kiswahili
  • Uchumi
  • Michezo
  • Facebook
  • ChinaABC
  • Sayansi
  • Afya
  • Nchi zinazokalia kimya vita ya biashara zitaathiriwa baadaye

    (GMT+08:00) 2018-07-09 17:16:51

    Vita ya biashara iliyoanzishwa na Marekani imepata majibu ya nchi mbalimbali duniani. Baada ya Canada na Mexico kuongeza ushuru wa forodha kwa bidhaa za Marekani zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 12.6 na bilioni 3, tarehe 6 China ilianza kuongeza ushuru wa forodha wa bidhaa za Marekani zenye thamani ya dola za kimarekani bilioni 34, huku Russia pia ikitangaza kuongeza ushuru wa forodha kwa bidhaa za Marekani. Wakati huo huo, kuna nchi kadhaa zimekalia kimya na vitendo vya kujilinda kibiashara vya Marekani, na kuna siku zitaathiriwa.

    Katika vita hiyo, hakuna wapita njia na watazamaji, nchi zote ni washiriki. Gazeti la Nikkei Asian Review la Japan tarehe 7 limetoa ripoti ikionya kuwa, vita ya biashara iliyoanzishwa na Marekani itasababisha uchumi wa dunia kudidimia, na nchi zilizoendelea zinapaswa kuishawishi serikali ya Rais Trump kutambua umuhimu wa utaratibu wa biashara huria kwa kauli moja.

    Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi tarehe 5 alipokutana na waandishi wa habari na mwenzake wa Austria, alisema China inasusia kitendo cha kujilinda kibiashara, kwa ajili ya kulinda maslahi ya pamoja ya nchi mbalimbali duniani zikiwemo nchi za Umoja wa Ulaya, na sasa China iko mstari wa mbele katika vita ya biashara, haipendi kupigwa na nchi nyingine kinyemelea.

    Lengo la serikali ya Marekani kuanzisha vita ya biashara si kama tu ni kuzuia maendeleo ya China, bali pia ni kumaliza utandawazi wa uchumi. Vita hiyo itadhuru maslahi ya nchi mbalimbali duniani. Kwa mfano shirika la magari la Fiat Chrysler ambalo ni moja ya mashirika matatu makubwa zaidi ya Marekani, na lina viwanda 23 vyenye wafanyakazi zaidi ya 56,000 nchini Marekani, lakini kwa kweli shirika hilo ni shirika la kimataifa, kwani liliandikishwa nchini Uholanzi, makao makuu yake yako nchini Uingereza, na lina viwanda nchini Italia, China na Brazil. Ripoti iliyotolewa na chombo cha habari cha Marekani imesema, kama serikali ya Marekani itaongeza ushuru wa forodha kwa magari kutoka nchi za nje, faida ya shirika la Fiat Chrysler itapungua kwa dola za kimarekani milioni 860 kila mwaka.

    Kutokana na mafungamano ya kiuchumi, nchi yoyote ikianzisha vita ya biashara, nyingine zinapaswa kushirikiana na kujitahidi kupunguza athari ya vita hiyo kadiri iwezekanavyo, ili kupata mafanikio ya pamoja.

    Webradio
    Sauti
    6:00-7:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 1
    12:00-13:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 2
    20:00-22:00 (Afrika Mashariki)
    • FM 3A
    • FM 3B
    Maoni yako